DKT.TAX AONGOZA WAOMBOLEZAJI KUMUAGA MEJA JENERALI(MSTAAFU) CHARLES MBUGE LUGALO
Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Mheshimiwa Dkt.Stergomena Lawrence Tax (Mb) tarehe 16 Oktoba, 2024 katika Hospitali Kuu ya Jeshi Lugalo, jijini Dar es salaam ameongoza Maafisa, Askari, Watumishi wa Umma pamoja na waombolezaji, kutoa Heshima za Mwisho na kuuaga mwili wa Marehemu Meja Jenerali Mstaafu Charles Mbuge, aliyefariki Dunia tareh 12 Oktoba 2024 nchini India alipokuwa akipatiwa matibabu.
Miongoni mwa Viongozi walioungana na Waziri wa Ulinzi na JKT kumuaga na kutoa Heshima za mwisho kwa Marehemu Jenerali Mbuge, ni pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Bw. Albert Chalamila, Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali Jacob Mkunda, Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania, Luteni Jenerali Salumu Othman, Mkuu wa Majeshi Mstaafu Jenerali Venance Mabeyo, na Viongozi wakuu wa vyombo vya Ulinzi na Usalama na Taasisi nyingine za Serikali na Kiraia.
Mwili wa Marehemu Meja Jenerali Mstaafu Charles Mbuge umesafirishwa kuelekea Mkoani Mara tayari kwa mazishi tarehe 17 Oktoba.
Tranding News
Newsletter
Subscribe to our newsletter to get the latest news

