logo

MHANDISI KALIMBAGA ACHAGULIWA ‎RAIS MPYA WA ARMFA BARANI AFRIKA

Chama cha Mifuko ya Matengenezo ya Barabara Afrika (ARMFA) kimemchagua Mhandisi Rashid Selemani Kalimbaga wa Tanzania kuwa Rais wake mpya katika siku ya nne ya Mkutano Mkuu wa 22 wa mwaka, unaofanyika mjini Monrovia, Liberia.

Kalimbaga, ambaye ni Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Barabara Tanzania (Road Fund), anachukua nafasi ya Essaie Moussa Aubin wa Cameroon, rais anayemaliza muda wake.

‎.

‎Uchaguzi wake unaashiria mwanzo wa awamu mpya ya uongozi kwa taasisi hiyo ya bara inayoratibu na kuimarisha ufadhili wa matengenezo ya barabara katika nchi wanachama wa Afrika.

‎Akizungumza mara baada ya kuchaguliwa, Mhandisi Kalimbaga alisema kipaumbele chake cha kwanza kitakuwa kuboresha mifumo ya ukusanyaji wa fedha za matengenezo ya barabara, akibainisha kuwa mataifa mengi bado yanakabiliwa na changamoto ya upungufu wa rasilimali za kuendeleza miundombinu hiyo.

‎“Tuna changamoto ya upatikanaji wa fedha za kutosha za matengenezo, Ni lazima tuweke mifumo madhubuti itakayoongeza mapato ya barabara ili kuhakikisha barabara zetu zinatunzwa kwa ufanisi.” alisema Mhandisi Kalimbaga.

‎Aidha, alisisitiza kuwa kuimarisha mwonekano, ushirikiano na usajili wa ARMFA ndani ya Umoja wa Afrika (AU) kutabaki kuwa muhimu katika ajenda yake, akiendelea na juhudi zilizoanzishwa na watangulizi wake.

‎“Tunahitaji kuendeleza jitihada za kukifanya chama kijulikane na kusajiliwa kikamilifu ndani ya AU ili kutekeleza majukumu yetu kwa ufanisi zaidi,”

‎.

‎“Bila barabara hakuna maendeleo. Wajibu wetu ni kuhakikisha mitandao ya barabara barani Afrika inabaki kupitika ili wananchi wapate huduma na uchumi ukuwe.”alisema.

‎Bw. Kalimbaga alieleza kuwa kuchaguliwa kwake ni heshima kubwa kwa Tanzania, akisema anaamini atapata ushirikiano kutoka kwa mamlaka za ndani anapotekeleza majukumu yake ya bara.

‎Pia ameishukuru Liberia, mwenyeji wa mkutano huo, kwa ukarimu, maboresho ya miundombinu, na hatua inazoendelea kuchukua katika kupanua mtandao wa barabara nchini humo.

‎Aidha, ametoa wito kwa viongozi wengine waliochaguliwa ndani ya ARMFA kufanya kazi kwa pamoja ili kutatua changamoto zinazolikabili shirika hilo na kuimarisha ufanisi wa taasisi za barabara kote Afrika.

‎Mkutano huo wa siku tano, ulioanza tarehe 17 Novemba 2025, unatarajiwa ku

hitimishwa mapema leo.

Frank Jordan
12345 123
Follow Us
logo

© 2023 Jordan Media. All Rights Reserved. Designed by Lylical Popcorn