logo

HATUTAMUONEA HURUMA MTUMISHI YEYOTE ATAKAYE KUSUDIA KUFANYA UBADHILIFU WA FEDHA MRADI WA AFDP -WAZIRI JENISTA MHAGAMA

Serikali kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera,Bunge na Uratibu) imekabidhi vyombo vya usafiri pikipiki 23 (tatu zikiwa ni za miguu mitatu), na magari 11 vyenye thamani ya zaidi ya shilingi Bilioni 2 kwa taasisi na wizara zinazotekeleza Programu ya AFDP.

.

Vyombo hivyo vimekabidhiwa leo Machi 12,2024 na Waziri wa Nchi,Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera,Bunge na Uratibu) Mhe.Jenista Mhagama katika Mji wa Serikali Mtumba Jijini Dodoma ambapo aliambatana na Waziri wa Uchumi wa Buluu na Uvuvi Zanzibar Mhe.Shaaban Ali Othman, Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Sera, Uratibu na Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe. Hamza Hassan Juma, Naibu Waziri wa Kilimo Mhe.David Silinde na Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi Prof.Riziki Shemdoe.

.

Mhagama amesema Magari hayo yatatumika katika kusimamia na kufuatilia kwa karibu utekelezaji wa programu hiyo katika maeneo mbalimbali ikiwemo ujenzi wa miundombinu ya umwagiliaji,ujenzi na ukarabati wa majengo mbalimbali katika mashamba yanayomilikiwa na Wakala wa Mbegu za mazao ya kilimo (ASA) nk.

Kwa upande mwingine,Waziri Mhagama amewasisitiza wahusika wanaosimamia programu hiyo kuhakikisha wanazingatia thamani ya fedha itakayotumika katika mradi huo na kila fedha itakayowekwa katika mradi huo,itumike kwa kazi zilizokusudiwa.

.

"Hatutamuonea haya mtumishi Yeyote atakaye kusudia kufanya ubadhilifu wa fedha ya mradi huu ambayo watanzania wote wanaamini mradi huu unakwenda kuongeza chachu ya upatikanaji wa ajira,kuondoa umaskini na kukuza uchumi wa pato la mtu mmoja mmoja kwenye kaya.

.

"Tumejipanga na Mawaziri wenzangu kusimamia mradi huu ipasavyo na kwa thamani ya fedha iweze kuonekana" alisema Mhagama.

.

Aidha,Mhagama amesema malengo ya Programu hiyo ni kufikia kaya zenye kipato cha chini zipatazo laki mbili na sitini (260,000) kwa lengo la kuwaongezea kipato, lishe bora na usalama wa chakula, shughuli mbalimbali zinatekelezwa na Wizara, Taasis mbalimbali na halmshauri.

.

Kwa Upande wake Waziri wa Uchumi wa Buluu na Uvuvi Zanzibar Mhe.Shaaban Othman amesema kwa upande wao Tanzania Visiwani wataendelea kushirikiana na Tanzania Bara ili Kuhakikisha malengo ya serikali na ya taasisi zao yanafikiwa.

.

Aidha,Naye Naibu Waziri wa Kilimo Mhe.David Silinde(ambaye alimwakilisha Waziri wa Kilimo Mhe.Hussein Bashe) kwa upande wa Wizara ya Kilimo, programu ya AFDP inatekelezwa wizara hiyo Makao,TARI,ASA na TOSCI kwa lengo la kuleta mageuzi katika sekta ya Kilimo kwa kuleta tija na kuboresha uzalishaji mbegu bora za mahindi, alizeti nk.

#JordanMediaupdates

Frank Jordan
12345 123
Follow Us
logo

© 2023 Jordan Media. All Rights Reserved. Designed by Lylical Popcorn