logo

MAKADINALI 135 KUMCHAGUA PAPA MPYA MWEZI MEI 07,2025 VATICAN NCHINI ITALIA

Makadinali wa kanisa katoliki duniani wamechagua mwezi Mei 7 kama tarehe ya kuanza kongamano na kumchagua kiongozi mpya wa Wakatoliki bilioni 1.4 kote ulimwenguni.

.

Makadinali walio chini ya umri wa miaka 80 pekee ndio wanaoruhusiwa kupiga kura katika uchaguzi wa Papa.

.

Kwa sasa kuna makadinali 135 wanaostahili kushiriki katika uchaguzi ujao.

.

Makadinali hao, jumatatu hii wamefanya mkutano wa kwanza tangu mazishi ya Papa Francis, mikutano mikuu ni mikutano inayofanyika kila siku kufuatia kifo cha Francis ili kujadili mambo ya kanisa na maandalizi ya mkutano.

.

Siku ya jana Jumapili alasiri, baadhi ya makadinali walitembelea kaburi hilo la marumaru lenye maandishi “Franciscus” ili kutoa heshima kwa marehemu papa.

.

Mkutano huo utafanyika katika Kanisa la Sistine la Vatikani, ambalo linasalia kufungwa kwa wageni wakati wa siku hizo.

Frank Jordan
12345 123
Follow Us
logo

© 2023 Jordan Media. All Rights Reserved. Designed by Lylical Popcorn