logo

WAZIRI MKUU MSTAAFU WA ‎KENYA RAILA ODINGA AFARIKI DUNIA ‎

Aliyekuwa Waziri Mkuu wa Kenya na Kiongozi wa Chama Cha Orange Democratic Movement (ODM) Bw. Raila Odinga, amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 80 mara baada ya kupata tatizo la mshtuko wa moyo ambapo alikuwa akipatiwa matibabu nchini India.

‎.

‎Taarifa za kifo chake zimethibitishwa asubuhi ya leo.

‎Maisha ya Raila kisiasa yanachukua zaidi ya miongo minne, kwani ni mhusika mkuu katika vita vya Kenya vya demokrasia ya vyama vingi na aliwekwa kizuizini mara kadhaa wakati wa utawala wa Rais Moi.

‎Baada ya demokrasia kurejeshwa, alikuwa mbunge wa Lang’ata mwaka wa 1992 na tangu wakati huo amekuwa kitovu cha siasa za Kenya.

Raila amewahi kuwa Waziri wa Nishati, baadaye wa Barabara na Makaazi na alikuwa Waziri Mkuu wa Kenya katika serikali ya mseto ya mwaka 2008 na Rais Mwai Kibaki.

‎Amewania urais mara tano - mwaka wa 1997, 2007, 2013, 2017 na 2022 - akibaki mmoja wa viongozi wa upinzani wenye ushawishi mkubwa na mtetezi wa mageuzi nchini Kenya.

Frank Jordan
12345 123
Follow Us
logo

© 2023 Jordan Media. All Rights Reserved. Designed by Lylical Popcorn