logo

MARIA MACHADO KIONGOZI WA UPINZANI VENEZUELA ASHINDA ‎TUZO YA NOBEL YA AMANI 2025 NCHINI NORWAY

Kiongozi wa upinzani wa Nchini Venezuela Bi. Maria Corina Machado, ameshinda Tuzo ya Nobel ya Amani (Nobel Peace Prize) kwa mwaka huu 2025,kwa kukuza haki za kidemokrasia kwa watu wa taifa hilo.

‎Kamati ya Nobel ya Norway imesema, María Corina Machado amesaidia kuweka moto wa demokrasia ukiwaka dhidi ya giza linaloongezeka.

‎.

‎Ikitangaza tuzo hiyo katika sherehe maalum mjini Oslo leo tarehe 10 mwezi Oktoba,2025, kamati hiyo imesifu mapambano ya Machado kufikia mabadiliko ya haki na amani kutoka kwa udikteta hadi demokrasia.

‎.

‎Kwa upande wa Mwenyekiti wa Kamati ya Nobel, amesema hana uhakika kama Machado ataweza kuhudhuria hafla ya zawadi nchini Norway mnamo mwezi Desemba mwaka huu.

‎.

‎Naye Rais wa Marekani Donald Trump hakuficha hamu yake ya kupata Tuzo ya Amani ya Nobel, lakini haikuwezekana angetunukiwa tuzo ya mwaka huu kwa sababu ya mchakato wa uteuzi.

‎.

‎Aidha, Tuzo za Nobel katika Kemia, Fizikia, Dawa na Fasihi pia zilitolewa wiki hii.

Frank Jordan
12345 123
Follow Us
logo

© 2023 Jordan Media. All Rights Reserved. Designed by Lylical Popcorn