logo

MCHANGO WA SEKTA YA BIASHARA KATIKA PATO LA TAIFA KWA MWAKA 2024 ASILIMIA 8.6-WAZIRI JAFO

Waziri wa Viwanda na Biashara,Mhe. Dkt. Selemani Jafo (Mb) amesema Mchango wa Sekta ya Biashara katika Pato la Taifa kwa mwaka 2024 ulikuwa asilimia 8.6 ikilinganishwa na asilimia 8.4 mwaka 2023.

.

"Kasi ya ukuaji wa Sekta ya Biashara ilikuwa asilimia 4.8 mwaka 2024 ikilinganishwa na asilimia 4.2 mwaka 2023" alisema.

.

Waziri Jafo ameyasema hayo leo Mei 15,2025 jijini Dodoma wakati akizungumza na waandishi wa Habari kuhusu Mafanikio ya miaka minne ya Serikali ya awamu ya Sita katika Wizara hiyo.

.

Amesema Hadi kufikia Machi, 2025, jumla ya shilingi bilioni 5.7 sawa na asilimia 97 ya fedha zote za fidia zililipwa kwa wafidiwa 528 kati ya wafidiwa 595.

.

"Ukamilishaji wa zoezi wa kiasi kilichobaki cha shilingi milioni 194.3 unaendelea kwa wafidiwa 67 waliobaki" alisema Waziri Jafo.

.

Amesema Mradi wa makaa ya mawe Katewaka upo katika hatua za mwisho za kuanza utekelezaji, una akiba ya tani milioni 100 na uwezo wa kuzalisha tani milioni 1.5 kwa mwaka kwa muda wa miaka 100.

.

"TBS pia imesajili bidhaa 6,677 za chakula na vipodozi kutoka nje na kufanya kaguzi za shehena 131,072 kabla ya kuingizwa nchini, bidhaa 286,709 baada ya kuingia na magari 176,122 yaliyotumika" alisema Dkt. Jafo.

.

Aidha, amesema Tanzania ina jumla ya viwanda vinne vya kuzalisha bidhaa za vioo ambavyo vinatumia malighafi kama dolomite, silca sand, limestone na feldspar katika kuzalisha bidhaa, na malighafi hizo zinapatikana nchini kwa zaidi ya asilimia 95.

Frank Jordan
12345 123
Follow Us
logo

© 2023 Jordan Media. All Rights Reserved. Designed by Lylical Popcorn