logo

DKT. TULIA AITAKA POSTA KUONGEZA KASI YA HUDUMA KWA JAMII

SPIKA wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt Tulia Ackson Amelitaka Shirika la Posta Tanzania Kuongeza Nguvu Zaidi Katika Kutoa Huduma Kwa Jamii Kwa Sababu Shirika hilo Limewezeshwa Na Suala La Anwani za Makazi.

Ackson Ameyasema Hayo Jana Mei 18,2023 Alipotembelea Maonesho Ya Mabanda Hayo yanayofanyika katika viwanja vya Bunge jijini Dodoma, ikiwa ni kuelekea uwasilishaji wa bajeti ya Wizara tarehe 19 Mei, 2023.

Amesema Amefurahishwa Na Maonesho Hayo Hususani Suala La Anwani za Makazi ambalo lilianza Mwaka Jana 2022 na Hadi Sasa limeweza kufikia Sehemu pazuri.

"Nitumie Fursa Kuwapongeza Kwa Juhudi Mbalimbali Wizara Hii Kwa Juhudi mnazozifanya Kwa Sababu Mtu Kujua Anwani yake Ni Jambo la Msingi" Amesema Ackson.

Spika Huyo Amesema Kwa wale Wananchi ambao Mpaka Hivi Sasa Bado Hawajajisajili au Hawajasajili Makazi Yao kwenye Mfumo Wa Anwani ya Makazi ni Muhimu Sana Kupata Anuani za Makazi Kwani zinasaidia kwenye Maendeleo.

"Anwani Zinasaidia Mtu kukufikia Kwa Urahisi Na Pia Zinakusaidia wewe kama Kuna Jambo umeagiza Mahali Basi Unaweza kumwambia Mtu uko Wapi na Unaishi Wapi" Amesema Spika Huyo.

Aidha, Ackson Ametoa Pongezi Kwa Shirika Hilo Kwa Kuwahudumia Wananchi Wote Kwa Kuhakikisha wanapata Kile Wanachohitaji Kupitia Mawasiliano.

Nae Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano na Mambo ya Kimataifa Bw. Elia Madulesi Amesema Kwa Upande Wa Posta Mfumo Wa Anwani upo Tayari na Kwa Hivi Sasa Kila Mtanzania anajulikana Alipo na atapata Huduma Yoyote Ile atakayoipata Kutokana na Kurahisishwa Kwa Huduma Ya Mawasiliano.

"Posta Tunasema Tunakufikia Hadi Nyumbani kwako Kwa Maana Tunajua Anwani Yako, Tunajua Ulipo kwahiyo Tunaweza kukufikishia Kwa Urahisi.

.

"Mwananchi haitaji Kuja Posta kututafuta, Sisi Ndio tutamtafuta, Kupitia Anwani za Makazi zinatuwezesha kukufikishia Huduma pale Ulipo" Alisema Madulesi.

#JordanMediaupdates

Frank Jordan
12345 123
Follow Us
logo

© 2023 Jordan Media. All Rights Reserved. Designed by Lylical Popcorn