logo

NAIBU WAZIRI UTUMISHI AIPA HEKO WIZARA YA UJENZI

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais-Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bw.Deus Sangu ameipongeza Wizara ya Ujenzi kwa utekelezaji wa miradi mbalimbali ya kimkakakati ikiwemo ujenzi wa daraja la J. P Magufuli lililozinduliwa jana Juni 19, 2025 na Mhe. Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan.

Pongezi hizo amezitoa leo, Juni 20, 2025 wakati alipotembelea banda la Wizara hiyo katika maonesho ya wiki ya Utumishi wa Umma yanayofanyika katika viwanja vya Chinangali park jijini Dodoma.

Amesema kuwa Wizara inafanya kazi nzuri zinazoonekana ikiwemo utekelezaji wa daraja hilo na miradi mingine ya barabara na madaraja inayoendelea kutekelezwa katika maeneo mbalimbali nchini.

Amesisitiza Wizara kutoa elimu kwa wananchi ikiwemo matumizi ya mfumo unaowezesha makandarasi wanawake wazawa kusajiliwa na kutambuliwa (WPU)ili kupatiwa miradi katika Serkta ya Ujenzi.

Aidha, ameahidi kutoa ushirikiano mkubwa katikati kutekeleza majukumu ya Wizara kwani miundombinu ya barabara na madaraja ndio chachu ya uchumi wa nchi.

Maonesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yalianza Juni 16, 2025 ambapo yanatarajiwa kuhitimishwa Juni 23, 2025 katika viwanja vya Chinangali Park jijini Dodoma na kuongozwa na kaulimbiu inayosema "Himiza matumizi ya mifumo ya kidijitali ili kuongeza upatikanaji wa taarifa na kuchagiza uwajibikaji"

Frank Jordan
12345 123
Follow Us
logo

© 2023 Jordan Media. All Rights Reserved. Designed by Lylical Popcorn