
QUEEN JULIETH LUGEMBE AREJESHA FOMU YA KUWANIA UBUNGE JIMBO LA UBUNGO
Mwanaharakati na kada wa Chama cha ACT-Wazalendo,Bi. Queen Julieth William Lugembe leo Agosti 27,2025 amerejesha rasmi fomu ya kuwania ubunge kupitia hicho katika Jimbo la Ubungo.
.
Hatua hii inampa nafasi ya kupeperusha bendera ya chama hicho kuelekea uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwaka huu.
Katika tukio hilo, Bi. Queen Julieth ameambatana na viongozi wa ACT-Wazalendo, wanachama pamoja na wafuasi wake, huku akisisitiza dhamira yake ya kuwatumikia wananchi wa Ubungo kwa uwazi, uwajibikaji na mshikamano wa kweli.
Aidha, Wananchi na mashabiki walijitokeza kwa wingi kumpokea na kumtakia kheri katika safari yake mpya ya kisiasa.
Tranding News
Newsletter
Subscribe to our newsletter to get the latest news