logo

MBUNGE NDUGULILE ATOA MABATI 660 KWA AJILI YA MADARASA 25 KIGAMBONI

MBUNGE wa Kigamboni Dkt.Faustine Ndugulile (Mb) leo tarehe 27 Mei, 2023 amegawa mabati 660 kwa ajili ya kuezeka madarasa 25 ambayo mabati yake yalikuwa yamechakaa na kuvuja.

.

Mabati hayo yaliyogharamiwa na mfuko wa Jimbo yamegharimu Tsh 58.9 millioni.

Katika salamu zake, Ndugulile amesema kuelekeza fedha za mfuko wa jimbo kwenye sekta ya elimu ni kuunga mkono juhudi za Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan za uwekezaji mkubwa kwenye sekta ya elimu nchini. Kigamboni ni wanufaika wa fedha za UVIkO Tsh 800 millioni, kapu la Mama Tsh 200 millioni na mradi wa Boost Tsh 1.5 billioni.

Hafla ya kukabidhi mabati hayo kwa walimu wakuu ilifanyika katika Ofisi za Halmashauri ya Manispaa ya Kigamboni na kuhudhuriwa na Mstahiki Meya Mhe Ernest Mafimbo, Waheshimiwa madiwani, Mkurugenzi wa Halmashauri Ndugu Erasto Kiwalle, watendaji wa Manispaa na walimu wakuu wa shule husika.

#JordanMediaupdates

Frank Jordan
12345 123
Follow Us
logo

© 2023 Jordan Media. All Rights Reserved. Designed by Lylical Popcorn