logo

WAZIRI BASHE: TUNAKABILIWA NA MATAPELI KWENYE SEKTA YETU YA KILIMO

Waziri wa Kilimo Mhe.Hussein Bashe Amesema Kwenye Sekta Ya Kilimo Kwa Hivi Sasa wanakabiliwa Na Changamoto ya Matapeli Kitu ambacho Ni Tatizo Kubwa, Na Tatizo Hilo linakwenda kuua Biashara Yetu Nje Ya Nchi Kwa Sababu Biashara Yoyote Ile Kitu Cha Kwanza Ni Uaminifu.

.

"Wapo Wafanyabiashara wanakopeshwa Na Benki Sio Kwa Sababu ya Vitu walivyokuwa navyo Ni Kwa Sababu ya Uaminifu waliyokuwa nayo kwenye Taasisi Ya Fedha" Amesema Bashe.

.

Bashe Ameyasema Hayo Leo Julai 14,2023 Alipokuwa Kwenye Mkutano wa Wafanyabiashara Na Wadau wanaouza Mazao Ya Kilimo Ndani Na Nje Ya Nchi Uliofanyika Leo Katika Ukumbi Wa Mabeyo Jijini Dodoma.

.

Amesema Kutokana na Hilo wameharibu Biashara kwenye Baadhi Ya Nchi Ikiwemo Uturuki kwa Sababu Ya Watu wawili Ambao walikuwa wanaaminiwa Na wanunuzi Nje Ya Nchi, Na wakapewa Malipo Ya mwanzo.

.

"Sasa Hivi Tuna Tatizo na Baadhi Ya Wafanyabiashara Ambao wamesajiliwa na Wenzetu Wa India Ya Kwamba Hawa Ni wanunuzi Kutoka Nchini Tanzania wanaotuuzia mazao Mbalimbali, Wamelipwa Fedha hawapeleki Mazao" Amesema Bashe.

.

Waziri Huyo Amewaomba Wakulima Wote Nchini wajisajili kwenye Mfumo Maalum Ambao Serikali inasajilia Wakulima wake Ili waweze kutambulika Zaidi Kupitia Idadi Yao na Shughuli wanayoifanya.

.

"Hata Kama Una Shamba La Parachichi, Nenda kajisajili kwenye Mfumo Huo, Mpaka Sasa Tumeshasajili Wakulima Milioni 3 na Lengo Letu kusajili Wakulima Milioni 7, Na tunawafahamu Kwa Majina na Sehemu Walipo" Amesema Bashe.

.

Aidha, Bashe Amesema Kwa hivi Sasa wameanza Kujenga Maghala Takribani 25 Katika Mkoa Wa Ruvuma Pekee na Maghala Hayo Yatakuwa yanapatikana Kwa Ajili ya Wakulima Wadogo na Wafanyabiashara Ili waweze Kununua Mazao na Kupata Kituo kwa Ajili Ya Kuhifadhi Mazao.

#JordanMediaupdates

Frank Jordan
12345 123
Follow Us
logo

© 2023 Jordan Media. All Rights Reserved. Designed by Lylical Popcorn