logo

RAIS SAMIA: WANAFUNZI WATAPATA UFADHILI WA MASOMO NCHINI TANZANIA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Dkt.Samia Suluhu Hassan Amesema Makubaliano waliyoyafanya Baina Ya Tanzania Na Hungary yanakuja na mbinu mpya ambapo wanafunzi watapata ufadhili wa masomo wakianza na wanafunzi watano kutoka Hungary kuja kusoma vyuo vya Tanzania na wanafunzi 30 wa Tanzania kwenda kusoma katika vyuo vya Hungary.

.

Rais Samia Ameyasema Hayo Leo Julai 18,2023 Jijini Dar Es Salaam Wakati Rais Wa Jamhuri Ya Hungary Mhe.Katalin Novak akiendelea Na Ziara Yake Ya Siku Nne Nchini Tanzania.

.

Amesema Katika upande wa utalii kwa miaka mingi Tanzania na Hungary wana ushirikiano mzuri mathalani katika mwaka 2022, Tanzania imepata watalii 7,188 kutoka Hungary.

.

"Tunaamini baada ya ziara yako tutapata watalii wengi kutoka nchini Hungary. Pia, tunawakaribisha wawekezaji kutoka Hungary kuja kuangalia fursa za kuwekeza katika sekta ya utalii" Amesema Samia.

.

Kwa Upande mwingine, Rais Samia Amesema Kuhusu usawa wa kijinsia na uwezeshaji wa wanawake, katika majadiliano yao wamekubaliana kuweka masuala ya uwezeshaji wanawake, masuala ya jinsia na maendeleo ya watoto kuwa ajenda kubwa katika mashirikiano yao mbalimbali.

.

Aidha, Amesema Kwa niaba ya Serikali, ameahidi kutoa ushirikiano na kuisaidia nchi ya Hungary na Jumuiya ya Wafanyabiashara wanaopenda kuja kuwekeza nchini Tanzania.

.

Naye Rais wa Jamhuri ya Hungary, Mhe. Katalin Novak Amesema Makubaliano Hayo yametoa nafasi kwa wanafunzi wa Hungary kuja kusoma Tanzania na kujifunza lugha za Tanzania, watakuwa mabalozi wazuri wa kuitangaza Tanzania watakaporudi Hungary baada ya masomo yao.

.

Amesema Hungary wana programu zinazofadhiliwa na Serikali, kuna wanafunzi 12,000 kutoka nchi 19 wanaosoma Hungary kupitia programu hiyo wakiwemo Watanzania.

#JordanMediaupdates

Frank Jordan
12345 123
Follow Us
logo

© 2023 Jordan Media. All Rights Reserved. Designed by Lylical Popcorn