
ASKOFU MSTAAFU DKT.ERASTO KWEKA AFARIKI DUNIA
Askofu Mstaafu wa KKKT, Dayosisi ya Kaskazini Dkt. Erasto N. Kweka (89), amefariki dunia katika hospital ya Taifa ya Muhimbili (MNH), alipokuwa akipatiwa matibabu.
Hayati Dkt.Kweka, ambaye ametumikia Kanisa kwa zaidi ya miaka 40, alikuwa Askofu wa pili wa Dayosisi ya Kaskazini, akipokea nafasi hiyo baada ya kifo cha Askofu Dkt. Stephano Moshi na aliiongoza kuanzia mwaka 1977-2004, alipokabidhi kwa Askofu Dkt. Martin Shao.
Uongozi wa KKKT Dayosisi ya Kaskazini una masikitiko makubwa kutangaza kutwaliwa kwa baba Askofu Mstaafu Dk Erasto Kweka, kifo kimetokea leo, Novemba 25, 2023 saa nne asubuhi katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI)
Jordan Media Inatoa Pole Kwa Ndugu Jamaa Na Marafiki Kwa Msiba Huu Mzito, Bwana Ametoa na Bwana Ametwaa, Jina la Bwana lihimidiwe
#JordanMediaupdates
Tranding News
Newsletter
Subscribe to our newsletter to get the latest news