logo

MPIGA PICHA WA AL JAZEERA AUAWA KWA SHAMBULIO GAZA

Mpiga picha wa kituo cha Televisheni cha Al Jazeera ameuawa, na mkuu wa ofisi ya mtandao wa Kiarabu wa Ukanda wa Gaza alijeruhiwa siku ya Ijumaa Disemba 15,2023 wakati wa shambulio kusini mwa Gaza,

Al Jazeera imesema kuwa,limekuwa ni tukio la hivi punde katika msururu mrefu wa vifo vya waandishi wa habari katika vita hivyo.

.

Mpiga picha huyo aliyetambulika kwa jina la Samer Abu Daqqa, na Wael al-Dahdouh, mkuu wa ofisi hiyo, walikuwa wakiripoti athari za mashambulizi ya anga katika shule ya Umoja wa Mataifa iliyoko Khan Younis wakati wote wawili walijeruhiwa, mtandao huo ulisema.

.

Bw.al-Dahdouh aliiambia Al Jazeera kwamba aliweza kutoka nje ya eneo hilo na kutafuta msaada. Bwana Abu Daqqa alitokwa na damu hadi kufa kutokana na majeraha yake, kwani msaada wa matibabu wa dharura haukuweza kumfikia, mtandao huo ulisema.

.

Bwana Abu Daqqa mwenye umri wa miaka 45, alikuwa mwanahabari wa 13 wa Al Jazeera kuuawa tangu mtandao huo kufunguliwa mwaka 1996, kwa mujibu wa Al Jazeera.

Mazishi yake yalifanyika Khan Younis siku ya Jumamosi. Al Jazeera imerusha sehemu ya mazishi yake, ambapo Bw. al-Dahdouh alizungumza pamoja na wafanyakazi wenzake kadhaa, wanafamilia.

.

Bw. al-Dahdouh ameshutumu vikosi vya Israel kwa kulenga makumi ya waandishi wa habari, ofisi zao na familia zao.

"Tutaendelea kufanya kazi yetu kwa weledi bora na uwazi," licha ya kuwalenga waandishi wa habari, alisema. "Tutabeba ujumbe wetu."

.

Jeshi la Israel lilisema kuwa "halijawahi, na kamwe, kuwalenga waandishi wa habari kimakusudi," na inachukua "hatua zinazowezekana kiutendaji" kulinda raia na waandishi wa habari.

Khan Younis ni mojawapo ya maeneo matatu ambayo Israel imesema inalenga katika vita vyake vya kutokomeza Hamas kutoka Gaza.

#JordanMediaupdates

Frank Jordan
12345 123
Follow Us
logo

© 2023 Jordan Media. All Rights Reserved. Designed by Lylical Popcorn