logo

OKASH: WAZAZI TUWAPELEKE WATOTO WAKAPATE CHANJO

WITO Umetolewa kwa Wazazi Wote Nchini wenye watoto walio na umri Chini ya Miaka 5, kuhakikisha wanapeleka watoto wao katika vituo vya afya ili kupata chanjo.

.

Hayo Yamesemwa Na Mkuu Wa Wilaya Ya Bagamoyo Mhe.Halima Okash Leo April 29,2023 Alipotembelea Kituo Cha Afya Cha Wilayani Hapo.

.

Okash Amesema Katika Wilaya Yake wapo kwenye Kampeni ya Siku 7 kuhakikisha wanawafikia watoto wote walio chini ya miaka 5 walioko ndani ya Wilaya ya Bagamoyo Na kwa Halmashauri zote mbili.

.

Aidha, Mkuu Huyo Amewasisitiza Wazazi wote kushirikiana Na Serikali katika hilo Ili Kuhakikisha Watoto wanapata Chanjo Kwa Wakati.

#JordanMediaupdates

Frank Jordan
12345 123
Follow Us
logo

© 2023 Jordan Media. All Rights Reserved. Designed by Lylical Popcorn