
RAIS SAMIA ASHIRIKI MAADHIMISHO YA MIAKA 30 MAUAJI YA KIMBARI KIGALI NCHINI RWANDA
Matukio mbalimbali katika picha ni Maadhimisho ya miaka 30 tangu kutokea mauaji ya Kimbari Kigali nchini Rwanda.
.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt.Samia Suluhu Hassan ameshiriki katika Maadhimisho hayo ambapo alipata nafasi ya kutoa Heshima ya kuweka shada la maua kwenye eneo la Makaburi ya kumbukumbu ya mauaji ya Kimbari.
.
Katika tukio hilo,Rais Samia alikuwa ameambatana na viongozi mbalimbali wakimshuhudia Rais wa Rwanda Mhe. Paul Kagame akiwasha mwenge wakati wa kumbukumbu ya mauaji ya Kimbari Kigali nchini Rwanda.
Maadhimisho hayo ya miaka 30 yamefanyika katika Makumbusho ya Mauaji ya Kimbari, Kigali nchini Rwanda na kuhudhuriwa na viongozi kutoka nchi mbalimbali tarehe 07 Aprili, 2024.
#JordanMediaupdates
Tranding News
Newsletter
Subscribe to our newsletter to get the latest news