logo

CRDB YATOA ZAWADI ZA LAPTOP KWA WANAFUNZI BORA

MKURUGENZI Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela amewakabidhi zawadi ya laptop wanafunzi bora wa Shahada ya Benki na Fedha (Bachelor of Banking and Finance) kutoka Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM), Omary Singano (nafasi ya kwanza), Isaya Mpire (nafasi ya pili) na Joseph Lameck (nafasi ya tatu).

Benki ya CRDB ni mdhamini wa zawadi za wanafunzi bora wa fani hiyo na kwenye mahafali ya 47 yaliyofanyika Novemba 25 mwaka jana iliahidi kutoa kompyuta hizo kwa wahitimu watatu bora.

Tukio hilo la kukabidhi zawadi lilishuhudiwa na Mkurugenzi wa Rasilimali Watu wa CRDB, Godfrey Rutasingwa, Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mafunzo na Maendelwo Benki ya CRDB, Edith Mwiyombela, na Dkt Omary Fadhil, Mkuu wa Idara ya Udahili na Wateja wa hadhiri IFM.

@crdbbankplc

#JordanMediaupdates

Frank Jordan
12345 123
Follow Us
logo

© 2023 Jordan Media. All Rights Reserved. Designed by Lylical Popcorn