logo

MIAKA 60 YA MUUNGANO, IMELETA CHACHU YA MAGEUZI KATIKA SEKTA YA ELIMU TANZANIA -PROF.KITILA MKUMBO

Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais,Mipango na Uwekezaji, Mhe.Prof.Kitila Mkumbo amesema katika kipindi cha Miaka 60 ya Muungano kumekuwa na ongezeko la watoto waliofanikiwa kufika sekondari kutoka shule za msingi ambapo kwa mwaka 2000, ongezeko hilo lilikuwa chini ya 20% ukilinganisha na mwaka 1964 ilipokuwa 5% pekee.

.

Prof.Kitila ameyasema hayo April 17,2024 alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mafanikio katika wizara yake ndani kipindi cha miaka 60 ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania jijini Dodoma.

Aidha,Prof.Kitila ameweka wazi lengo la Serikali katika kuboresha sekta ya elimu, kuwa ifikapo mwaka 2025 nchi inatarajia kufikia asilimia 48 ya watoto wanaojiunga na elimu ya sekondari kutoka shule za msingi.

"Kwa takwimu za hivi sasa, tupo asilimia 70, Dira ya Maendeleo ya Taifa inayokuja, tutahitaji elimu ya msingi Tanzania iwe kwa Watanzania wote na wote lazima kufika sekondari kwa asilimia 100" alisema.

Frank Jordan
12345 123
Follow Us
logo

© 2023 Jordan Media. All Rights Reserved. Designed by Lylical Popcorn