logo

CHANDE: ENDELEENI KUFANYA KAZI KWA BIDII NA WELEDI

NAIBU Waziri Wa Fedha Na Mipango Mhe.Hamad H. Chande Ametoa Wito Kwa Watumishi Wa Ofisi Ya Taifa Ya Takwimu Kuendelea Kufanya Kazi Kwa Bidii Na Weledi huku wakizingatia Maadili Ya Utumishi Wa Umma Wakati Wote.

Ameyasema hayo Leo Mei 03,2023 Jijini Dodoma Alipokuwa Akifungua Mkutano Wa Wafanyakazi Wa Ofisi Ya Taifa Ya Takwimu Katika Ukumbi Wa Jenerali Venance Mabeyo.

Chande Amesema Serikali inawatahadharisha Watumishi Ambao hawatozingatia Maadili Kuwa Haitawavumilia Kwani Kukosa Maadili Sio Tu, kunadhorotesha Uzalishaji na Utoaji Wa Huduma Bali Pia kunatia Doa Sifa nzuri ya Utumishi Wa Umma na Inakuwa Kero Kwa Wananchi.

"Ninyi Wenyewe mnaona Mifano Hapa Nchini Na Ulimwenguni Kote, Mtu akiwa Mfanyakazi kama Amefanya Kosa Kwa Jamii Kila Mmoja Anasema Mtumishi Wa Umma Huyu Lakini Mwengine Wala Watu hawashughuliki.

"Hata Leo Hii Wewe Ukipanda Gari Lako watasema Mtumishi Wa Umma Huyo ingawa Sio Kosa, Nawaombeni Sana Tuendelee kudumisha Maadili Yetu na Kufanya Kazi Kwa uweledi" Amesema Chande.

Naibu Waziri Huyo Amesema Serikali itazitumia Takwimu za Sensa zilizotolewa Mwaka Jana 2022 Kwa Ufanisi Mkubwa, Na Hawatoweza Kuziacha Kuziacha Kazi ambayo imefanywa Kwa Nguvu na Gharama zote ipite Bure.

Aidha, Chande Ametoa Pongezi Kwa Makamisaa Wa Sensa Mhe. Anna Makinda Kwa Upande Wa Tanzania Bara, Na Mhe. Balozi Mohammed Hajj Hamza Kwa Tanzania Visiwani, Bodi Ya Usimamizi Ya NBS Na Menejimenti Ya Ofisi Ya Taifa Ya Takwimu (Chini Ya Mtakwimu Mkuu Wa Serikali Dr. Albina Chuwa) Na Watumishi Wote.

Nae Kamisaa Wa Sensa Ya 2022 Mhe. Anna Makinda Amewataka Watumishi Hayo Kujiandaa Kwa Ajili Ya Ziara Ya Mikoa Yote Upande Wa Tanzania Bara ikiwa Ni Sehemu ya Utekelezaji Wa Mpango Kazi Wa Usambazaji Na Mafunzo ya Matumizi ya Matokeo Ya Sensa ya Mwaka 2022.

Makinda Amesema Katika Sensa Ya Mwaka 2022 Suala la Usambazaji Wa Matokeo Ya Sensa limepewa Kipaumbele ndio Maana Serikali ikaanda Mpango Kazi Wa Usambazaji Na Mafunzo Kwa Matumizi ya Matokeo Ya Sensa Ili Kuhakikisha Lengo la Kufanya Sensa linatimia ambayo ni kuipatia Nchi Yetu ambazo zitakuwa Dira ya Kufanya Maamuzi Ya Maendeleo Yetu na kusaidia kupima Utekelezaji Wa Mpango na Programu Mbalimbali za Maendeleo ya Kitaifa, Kikanda Na Kimataifa.

#JordanMediaupdates

Frank Jordan
12345 123
Follow Us
logo

© 2023 Jordan Media. All Rights Reserved. Designed by Lylical Popcorn