
AWESO ASHUHUDIA UTIAJI SAINI USANIFU MRADI WA MAJITAKA DODOMA
WAZIRI wa Maji Mhe Jumaa Aweso (Mb) ameshuhudia utiaji saini wa makubaliano ya usanifu wa ujenzi wa mradi wa majitaka katika jiji la Dodoma utakaosimamiwa na Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dodoma (DUWASA).
Usanifu wa mradi huo mkubwa utahusisha ujenzi wa mabwawa 16 ambayo yatakuwa na uwezo wa kutibu maji lita milioni 20 na awamu ya kwanza ya usanifu itafanyika kwa miezi 13 kwa gharama ya shilingi bilioni 12.
Aidha, Waziri Aweso amesema mfumo wa majitaka ni muhimu na uwekewe miundombinu mizuri ili kuweza kuepuka uchafuzi wa mazingira.
.
Waziri Huyo Amesisitiza jitihada kubwa lazima zifanyike na uwekezaji uongezwe kwa kiwango kikubwa kuhakikisha miundombinu ya majitaka inaenda sambamba na ujenzi wa miradi ya majisafi na usafi wa mazingira nchini.
Kwa upande wake Katibu Mkuu, Wizara ya Maji Mhandisi Nadhifa kemikimba amesema kutokana na ongezeko la watu katika jiji la Dodoma kumesababisha miundo mbinu ya majitaka kuelemewa hivyo usanifu ufanyike sambamba na kupatikana mkandarasi ili ujenzi wa mradi uanze.
@jumaa_aweso
#JordanMediaupdates
Tranding News
Newsletter
Subscribe to our newsletter to get the latest news