
CHADRON'S HOPE FOUNDATION YAWAFIKIA WANAWAKE 70 JIJINI DAR ES SALAAM
Mwanzilishi na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Chadron's Hope Foundation (@chadronfoundation) Bi.Elly Kitaly amesema kupitia mradi huo,mpaka hivi sasa wameweza kuwafikia wanawake 70, na kwa ujumla wao timu nzima iliyokuwepo kwenye semina hiyo ni takribani watu 120.
.
"Semina hii imekuwa ni muendelezo wa semina mbalimbali tulizokuwa tukizifanya, na tunatarajia tarehe 02 mwezi Novemba,2024 tutakuwa na semina inayogusa masuala ya wanawake na pia tutazungumzia masuala ya ukatili wa wanawake" alisema Elly.
.
Elly Kitaly ameyasema hayo Oktoba 19,2024 alipokuwa kwenye Semina ya "MAMA MWEMA" iliyofanyika Bunju jijini Dar Es Salaam katika Ukumbi wa L Square Villa Park ambapo ilijumuisha wazazi wenye watoto wenye ulemavu wa ukuaji, na ilijikita katika kuwapa elimu ya fursa za kiuchumi ili waweze kuwahudumia watoto wao na pia kujihudumia wao.
Tranding News
Newsletter
Subscribe to our newsletter to get the latest news