
RAIS WA RWANDA ANASEMA HAJUI KAMA WANAJESHI WA NCHI YAKE WAKO DRC
Rais wa Rwanda Paul Kagame kwenye mahojiano aliyoyafanya na chombo cha habari cha CNN leo February 03,2025 amesema kuwa, hajui kama wanajeshi wa nchi yake wako mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), ambako mapigano kati ya kundi la waasi la M23 na wanajeshi wa Kongo yamesababisha vifo vya zaidi ya watu 700 na maelfu kujeruhiwa siku za hivi karibuni.
Sehemu kubwa ya jumuiya ya kimataifa inaamini kuwa Rwanda inawaunga mkono waasi wa M23, waliodai kuuteka mji wa Goma mashariki mwa Kongo wiki iliyopita.
.
Wataalamu wa Umoja wa Mataifa wanaamini kuwa takribani wanajeshi 3,000 - 4,000 wa Rwanda wanawasimamia na kuwaunga mkono wapiganaji wa M23 mashariki mwa DRC, wakiwazidi wanajeshi wa kundi hilo la waasi nchini humo.
.
Katika mahojiano hayo pia, Kagame aliulizwa kama kuna wanajeshi wa Rwanda ndani ya DRC.
.
“Sijui, Kuna mambo mengi sijui. Lakini ukitaka kuniuliza, kuna tatizo huko Kongo ambalo linahusu Rwanda..? Na kwamba Rwanda ingefanya lolote kujilinda..? Ningesema 100%," alisema Kagame.
.
Aidha, Kagame amekitaja chama cha Democratic Forces for the Liberation of Rwanda (FDLR), mojawapo ya makundi makubwa ya kigeni yenye silaha yanayofanya kazi nchini DRC, "tishio lililopo" kwa Rwanda.
.
Alidai kuwa kundi hilo lilijumuishwa kikamilifu katika jeshi la Kongo, akipendekeza kuwa serikali zingine katika eneo hilo pia zinaunga mkono kundi la waasi.
Tranding News
Newsletter
Subscribe to our newsletter to get the latest news